Kiswahili kinafundishwa kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu nchini humo, lakini uhaba wa walimu stadi na vitabu bado ni changamoto.
Kuna shirika mmoja la binafsi linalojitolea kuwapa wanafunzi wa chuo kikuu mafunzo ya ziada ya kiswahili ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu wenye ujuzi wa kutosha.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili, VOA ameripoti kuwa jana Jumatano jioni zaidi ya wanafunzi 150 waliofuatilia mafunzo hayo walikabidhiwa vyeti kwa kukamilisha mafunzo yao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa SAPROS, Burundi Harerimana Pierre Claver iliojipa jukumu kuhakikisha inatoa mafunzo kwa vijana ili kuendeleza Kiswahili ameiambia VOA kwamba muamko huu wa vijana wa chuo kikuu katika kujifunza Kiswahili utakuwa ni ushahidi wa kutosha kwa wale wanaodai kuwa Burundi ni jamii ya waswahili na Kiswahili ni lugha mama kwao.
Mmoja wa wanafunzi hao katika Chuo kikuu cha Burundi, anasema anaona raha kutumia lugha ya kiswahili. Anasema miaka iliyopitahapa Burundi kiswahili kilichukuliwa kama lugha ya wahuni,lakini sasakimepenya hadi kwenye chuo kikuu.
Mzee Hussein Anzuruni ni mshahuri mkuu katika baraza la kiswahili Burundi (BALUKIBU) amesema, kiswahili kama somo sasa kinafundishwa kuanzia shule za msingi, hadi kwenye elimu ya juu.
Mwaka wa 2014lugha ya Kiswahili iliidhinishwa na bunge kama lugha ya kikanda. Lakini ufundishwaji wake bado unakumbwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitabu na walimu stadi.
Mhadhiri Dorothe Nshimimana, anafundisha Kiswahili kwenye vyuo mbali mbali vya Burundi kwa miaka 24 sasa. Anachukuliwa kama mtetezi nambari moja wa Kiswahili sanifu
Hadi sasa takriban vijana 2000 walifuzu mafunzo ya kiswahili kupitia Sapros Burundi.Idadi kubwa kati yao wako mstari wa mbele kufundisha somo la kiswahili ktk shule nyingi za sekondani nchini kote, amesema mhadhiri huyo.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Haidallah Hakizimana, Burundi.