Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 17:55

Kiraithe: Kenya iko salama


Wapelelezi wakagua eneo la mripuko ndani ya kanisa la God's House of Miracles International Church in Nairobi, kufuatia shambulio la gruneti April 29, 2012

Polisi wa Kenya wanakaribia kumtambua aliyehusika na shambulio dhidi ya kanisa moja mjini Nairobi iliyosababisha kifo cha mtu mmoja.

Polisi nchini Kenya wanaendelea na uchunguzi wa mripuko uulotokea katika kanisa la "God's House of Miricales International" Jumapili, lililosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 16 kujeruhiwa.

Msemaji wa polisi Eric Kiraithe ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wanauhakika katika muda wa saa 48 hadi 72 wataweza kumtambua aliyehusika na shambulio hilo lililotokea wakatti waumini walikua wanahudhuria misa ya Jumapili.

"Tuko na fununu, lakini kama amefadhiliwa na kundi hili au lingine baado hatujapata mwangaza.Tuko na mshukiwa lakini hatuna hakika kuhusu mambo mengi kuhusiana nae. Tuna fununu juu ya hasa yeye ni nani."

Waathiriwa wamelaani kitendo hicho, na madaktari wa Kenyatta Hospital wanasema watu 9 kati ya walolazwa hospitali wako katika hali nzuri.

Maafisa wa serikali wamewatembelea waathiriwa, hospitali akiwemo Makamu rais Kalonzo Musyoka ambae amelaani kitendo hicho akikieleza kuwa ni ugaidi, na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea

XS
SM
MD
LG