Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:41

Kipyegon wa Kenya ashinda dhahabu katika mbio za mita 1,500 mjini Budapest


Faith Kipyegon (Kulia) aliposhinda dhahabu katika fainali za mbio za mita 1,500 mjini Budapest, Hungary. Agosti 22, 2023.
Faith Kipyegon (Kulia) aliposhinda dhahabu katika fainali za mbio za mita 1,500 mjini Budapest, Hungary. Agosti 22, 2023.

Mwanariadha nyota raia wa Kenya, Faith Kipyegon, aliandikisha historia Jumanne kwa kushinda dhahabu yake ya tatu tangu alipoanza riadha, katika mbio za mita 1,500 mjini Budapest, Hungary, akimaliza mbio hizo kwa dakika  3, sekunde 54 na nukta 87.

Kipyegon, bingwa mara mbili wa Olimpiki , hajashindwa kwa muda wa miaka miwili mfululizo.

Akiwa bado na umri wa miaka 29, Budapest ni Mashindano yake ya sita ya Dunia, na sasa ana tuzoi tatu za dhahabu, mbili za fedha.

“Ninashukuru kwa kuvunja rekodi za dunia,” alisema Kipyegon. "Nilikimbia mbio zangu," aliongeza. "Sote tulikuwa na nguvu kwenye fainali. Siku hizi ukitaka kushinda 1500m lazima kukimbia kwa dakika 3:55 na chini. Zilikuwa mbio za kasi na nina furaha sana niliweza kutetea taji langu."

Muethiopia Diribe Welteji mwenye umri wa miaka 21 alikuwa wa pili, huku Sifan Hassan wa Uholanzi, akichukua nafasi ya tatu.

Kipyegon na Hassan huenda wakamenyana tena baadaye wiki hii wakati wote wawili wakikimbia mbio za mita 5,000.

Forum

XS
SM
MD
LG