Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 05:58

Kipsang aongoza ushindi wa Wakenya Frankfurt


Wanariadha wa Kenya katika mbio za Boston Marathon, April 18, 2011
Wanariadha wa Kenya katika mbio za Boston Marathon, April 18, 2011

Ushindi wa Kipsang mwaka huu ulivunja rekodi aliyoweka katika ushindi wake wa mwaka jana kwa dakika nzima

Mwanariadha Wilson Kipsang wa Kenya ameshinda mbio za marathon za Franfurt Jumapili katika muda wa saa 2, dakika 3 na sekunde 41, ikiwa ni sekunde tatu nje ya rekodi ya dunia inayoshikiliwa na Mkenya mwingine Patrick Makau.

Wakenya walichukua nafasi 10 kati ya 11 za juu katika mbio hizo ambazo wanariadha 15 walimaliza chini ya saa 2 na dakika 10.

Mwanadada Agnes Kiprop wa Kenya alishinda nafasi ya pili upande wa wanawake katika muda wa saa mbili, dakika 23 na sekunde 52 ambapo Mamitu Daska wa Ethiopia alichukua nafasi ya kwanza katika muda wa saa 2, dakika 21 na sekunde 57.

Levy Matebo naye wa Kenya alishika nafasi ya pili upande wa wanaume katika muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 15 akifuatiwa katika nafasi ya tatu na Mkenya mwingine Philip Sanga ambaye alimaliza katika muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 23.

Nafasi zote nyingine zilizofuata hadi nambari 11 zilishikwa na Wakenya isipokuwa nafasi ya nane ambaye ilishikwa na mwanariadha kutoka Ethiopia.

XS
SM
MD
LG