Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:58

Kiongozi wa upizani Zimbabwe akihama chama chake


Nelson Chamisa akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari Agosti 27, 2023. Picha na Zinyange Auntony / AFP
Nelson Chamisa akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari Agosti 27, 2023. Picha na Zinyange Auntony / AFP

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Zimbabwe, Nelson Chamisa ametangaza kujiuzulu kutoka chama chake siku ya Alhamisi, miezi michache baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa rais, akilalamikia “vitisho na ghasia” zinazofanywa na utawala.

Katika taarifa yake, Chamisa mwenye umri wa miaka 45 alisema “ Hii ni rasmi, iko mikononi mwangu , ninawaarifu wananchi wenzangu wa Zimbabwe and dunia , kwamba, kuanzia sasa hivi, mimi sijihusishi tena na CCC”.

“Wazo msingi la CCC limehujumiwa, limeshushwa hadhi, limeporwa na ZANU-PF kupitia unyanaysaji wa taasisi za Taifa,” amesema, akikishutumu chama tawala cha rais Emmerson Mnangagwa kwa kuwa na mbinu chafu.

Uamuzi huo wa kushangaza umetolewa baada ya Mnangagwa mwenye umri wa miaka 81 kushinda mhula wa pili katika uchaguzi wa rais, na kumshinda kiongozi wa Chama cha Citizens Coalition for Change (CCC), katika uchaguzi ambao pia umekipa chama tawala cha ZANU-PF idadi kubwa ya wabunge.

Wafuatiliji uchaguzi wa kimataifa wamesema upigaji kura haukuwa na viwango vya kidemokrasia, na mivutano ya kisiasa imeongezeka tangu wakati huo.

Akijulikana kwa jina la “Mamba” Mnangagwa aliingia madarakani kwa mara ya kwanza baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani kiongozi mkongwe Robert Mugabe mwaka 2017.

Chamisa alionekana akilitumia jina la utani la Mnangagwa, akitangaza: “Nimekataa kuongelea mtoni na Mamba mwenye njaa. Tunataka kujiondoa kutoka kwa wanasiasa wadanganyifu”

Kwa muda mrefu chama cha ZANU-PF kimekuwa kikishtumiwa kwa kutumia mahakama kuwalenga wapinzani wa kisasa na kuwanyamazisha.

Chama cha ZANU-PF kimepata viti 177 kati ya 280 katika bunge la taifa wakati chama CCC kimepata viti 104 baada ya uchaguzi huo wa Agosti 23.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG