Wachimbaji hao walikwama baada ya mkasa huo kutokea kwenye mgodi uliopo takriban kilomita 270 mashariki mwa mji mku wa Harare. Mangwana ameongeza kusema kwamba wachimbaji wote waliokwama wameokolewa, ingawa operesheni hiyo ilicheleweshwa kutokana ardhi isiyo imara, kulingana na kampuni ya Matallon Gold, inayomiliki mgodi wa Redwing.
Video iliorushwa kwenye mtandao wa X na Mangwana inawaonyesha wachimba madini hao wakiwa wamefunikwa na matope, huku wakishangiliwa na kundi dogo la watu, karibu na eneo la tukio.
Forum