Msemaji wa polisi Rae Hamoonga amesema leo kwamba kiongozi wa chama cha upinzani cha National Democratic, Saboi Imbolea anaendelea kushikiliwa, na kwamba amefahamishwa kwamba matamshi yake huenda yakatumiwa dhidi yake katika mahakama. Hamoonga ameendelea kusema kwamba Imbolea alikamatwa kutokana na kumkosoa mkurugenzi wa habari kwenye ofisi ya rais, Clayson Hamasaka kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mwaka 2021, sheria mpya ya kudhibiti mitandao ilipitishwa nchini Zambia chini ya chama tawala cha wakati huo cha Patriotic Front. Hata hivyo wakosoaji wanasema kwamba sheria hiyo inatumiwa kuminya uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari pamoja na haki ya faragha.