Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:53

Kiongozi wa Upinzani Uganda Boby Wine 'Apigwa risasi na polisi.'


Bobi Wine (katikati), akitoa hotuba akiwa na binti yake Suubi na mtoto wake wa kiume Shadrack Mbogo huko Kampala on January 26, 2024. Picha na AFP
Bobi Wine (katikati), akitoa hotuba akiwa na binti yake Suubi na mtoto wake wa kiume Shadrack Mbogo huko Kampala on January 26, 2024. Picha na AFP

Mpinzani maarufu wa Uganda, Bobi Wine, alipigwa risasi kwenye mguu na polisi Jumanne katikati mwa nchi, imetangazwa katika ujumbe kwenye akaunti yake rasmi kwenye mtandao wa kijamii wa X.

"Rais wetu Bobi Wine amejeruhiwa kwa risasi mguuni na polisi huko Bulindo! Amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya dharura. Tutaliarifu taifa kuhusu hali yake," unasomeka ujumbe huo.

Video zilizobandikwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha Bobi Wine, akiwa na fahamu, na jeraha lenye damu kwenye mfupa wa tibia wa mguu wa kushoto, akiondolewa na wafuasi waliombeba mabegani mwao.

Bulindo iko takriban kilomita 20 kaskazini mwa mji mkuu, Kampala.

Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 42 aliyekuwa mwimbaji maarufu, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anaongoza upinzani dhidi ya utawala wa Rais Yoweri Museveni, kiongozi ambaye ameitawala Uganda tangu 1986.

Bobi Wine na mke wake Barbie Kyagulanyi
Bobi Wine na mke wake Barbie Kyagulanyi

Akiwa mkuu wa chama cha National Unity Platform (NUP), alikuwa mpinzani mkuu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021.

Mseveni, mwenye umri wa miaka 79, alichaguliwa tena kwa muhula wa miaka sita kwa asilimia 58 ya kura, kulingana na matokeo rasmi, akimshinda Bobi Wine (35%) ambaye aliushutumu uchaguzi huo kuwa ni "utapeli."

Bobi Wine aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani mara nyingi katika miaka ya hivi karibuni na mikusanyiko ya wafuasi wake imevunjwa mara kwa mara.

Filamu ya kumbukumbu "Bobi Wine: Rais wa Watu" inayosimulia kampeni yake ya uchaguzi wa 2021, iliteuliwa katika Tuzo za Oscars mwezi Februari 2024.

Forum

XS
SM
MD
LG