Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Ghannouchi ni miongoni mwa darzeni ya maafisa wa ngazi ya juu wa chama cha Ennahdha ambayo akaunti zao za benki zilishikiliwa na benki kuu ya Tuniasia mapema mwezi huu. Chama hicho hata hivyo kimeendelea kukanusha tuhuma dhidi ya mafisa wake.
Chama hicho kimedai kwamba lengo la tuhuma hizo ni kuondoa macho kwenye kura ya maoni ya kubadili katiba, iliyopangwa na rais Kais Saied kwa lengo la kuongeza mamlaka ya rais na kupunguza mamlaka ya bunge pamoja na waziri mkuu.
Wakosoaji wa rais wanasema kwamba anajaribu kuhalalisha mapinduzi. Nejib Chebbi ambaye pia ni kiongozi wa upinzani amesema kwamba anahofia kukamatwa kwa Ghannouchi baada ya kufanyiwa mahojiano baadaye Jumanne. Saied pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali yake wamelaumu chama cha Ennahdha kwa masaibu ya kisiasa yaliokumba taifa hilo mwaka uliopita.