Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:29

DRC kumchunguza Katumbi kama anatumia mamluki wa kigeni


Moise Katumbi Chapwe
Moise Katumbi Chapwe

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza uchunguzi kuhusiana na shutuma kwamba kiongozi wa upinzani nchini humo, Moise Katumbi, anatumia mamluki wa kigeni, maafisa wa Serikali walisema jana Jumatano.

Waziri wa Sheria, Thambwe Mwamba alisema kwamba serikali ina ushahidhi wa nyaraka kwamba wanajeshi kadhaa wa zamani wa Marekani hivi sasa wanafanya kazi ya kumlinda bwana Katumbi katika jimbo la Katanga.

Katumbi, ambaye aliwahi kuwa Gavana wa mkoa wa Katanga eneo la uchimbaji madini ya shaba, alijiondoa kwenye Serikali ya Joseph Kabila mwezi Septemba mwaka uliopita na kujiunga na upinzani.

XS
SM
MD
LG