Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:08

Kiongozi wa upinzani awataka wa-Libya wasilipize kisasi


Watu wanaolindamitaa yao kwa kuweka vituo vya ukaguzi katika mitaa inayo mpinga Gadhafi mjini Tripoli.
Watu wanaolindamitaa yao kwa kuweka vituo vya ukaguzi katika mitaa inayo mpinga Gadhafi mjini Tripoli.

Mahamoud Jibril amewaomba wa-Libya kutolipa kisasi wakati wasi wasi unaoongezekaq kutokana na kugunduliwa maeneo walouliwa watu wengi Tripoli

Wiki moja ilopita ghala ya kuhifadhi chuma illiyogeuzwa kuwa jela ya muda kuwashikilia maadui wa kanali Muammar Gadaffi, imekuwa sasa kuwa jumba lenye vifusi 50 ya watu walochomwa moto. Nje ya hapo kuna miili 8 kwenye nyasi, mwili mmoja ukiwa na mikono imefungwa nyuma.

Taswira hii ya kutisha iko kwenye uwanja ambao hadi hapo Jumanne, ulikua unadhibitiwa na kikosi maalum cha Khamis Brigade, katika mtaa wa wasomi unaodhibitiwa na mtoto wa Bw. Ghadaffi, Khamis. Mtu mmoja aliyenusurika alisema wakati vikosi vya waasi vilipokaribia, wanajeshi wa Ghadaffi waliwapiga risasi wafungwa wao, na hapo tena kuichomo moto miili hiyo.

Takriban kila siku, maeneo mengine ya mauwaji ya haliaki yanapatikana huko karibu na Tripoli.

Kutokana na habari hizo za kusikitisha mkuu wa Baraza la Kitaifa la Mpito NTC Mahmoud Jibril, aliwahutubia wananchi wa Libya kupitia televisheni ya taifa na kuwaomba wasilipize kisasi.

Mahmoud Jibril, kiongozi wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya
Mahmoud Jibril, kiongozi wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya

“Msijaribu kulipiza kisasi, au kuharibu mali ya watu, au kuwadhuru wageni wala kuwatesa wafungwa wa vita. Ninaahidi kwamba kuwa kila mfungwa atafanyiwa kesi ya haki.”

Kwa upande wake kundi la kutetea haki za kibinadam Human Rights Watch, lilitangaza Jumapili kwamba limeorodhesha maeneo mengine manne ambako palifanywa mauwaji ya watu wengi. Katika maeneo hayo miili 110 ilipatikana huko eneo moja likiwa karibu na jingo la wizara ya usalama wa ndani ya Libya.

Mkurugenzi wa Human rights watch Sarah Whitson, alisema ushahidi unaashiria kuwa vikosi vya Bw. Ghadaffi vilifanya kampeni ya mauwaji ya kiholela pale Tripoli ilipokuwa inaanguka mikononi mwa waasi.

Wakati huo huo wasi wasi umezuka juu ya hatima ya karibu watu 40 000 walofungwa na vikosi vya Libya na hadi hivi sasahawajulikani walipo.

Msemaji wa wapiganaji wa upinzani Kanali Ahmed Bani anasema zaidi ya watu wengine elfu kumi wameachiliwa huru kutoka jela za serikali tangu kuanguka kwa mji wa Tripoli wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG