Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:45

Kiongozi wa upinzani akamatwa Pakistan


Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif
Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif

Mamlaka nchini Pakistan mapema leo zimemkamata mwanasiasa wa upinzani wa siku nyingi kwa tuhuma za uchochezi, baada ya kumkosoa kiongozi wa kijeshi mwenye nguvu nchini humo .

Azam Swati ambaye pia ni seneta kutoka chama cha Pakistan Tehreek e Insaf cha waziri mkuu wa zamani Imran Khan amefikishwa kizimbani baada ya kukamatwa alfajiri nyumbani kwake mjini Islamabad.

Idara ya serikali ya kijasusi ya FIA imemshitaki chini ya sheria za mtandao baada ya kuandika ujumbe wa twitter dhidi ya jeshi la Pakistan pamoja na mkuu wake Generali Qamar Javed Bajwa.

Ujumbe wa Bajwa ulichochewa na uamuzi wa mahakama ya mji wa mashariki wa Lahore ya kuondolea mashitaka ya usafirishaji haramu wa fedha waziri mkuu Shehbaz Sharif pamoja na mwanawe wa kiume Hamza Shehbaz.

Malalamiko ya idara ya FIA dhidi ya Bajwa yalikuwa kwamba alihujumu taasisi za serikali kwa kutumia maneno ya uongo, suala ambalo huenda likachocheka maafisa au wanajeshi kufanya mapinduzi.

XS
SM
MD
LG