Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:54

Kiongozi wa Tunisia aapa kuachia madaraka 2014


Ghasia za Tunisia.

Rais wa Tunisia ameamuru majeshi ya usalama kuacha kutumia silaha dhidi ya waandamanaji na kutangaza kupunguzwa kwa bei za vyakula vikuu, kufuatia maandamano mabaya ya kupinga bei za vyakula na ukosefu mkubwa wa ajira.

Rais Zine El Abidine Ben Ali alitangaza hatua mpya katika tangazo la televisheni Alhamisi kati kati ya ya vurugu mbaya kuliko zote za katika miongo kadhaa.

Pia aliahidi uhuru zaidi wa vyombo vya habari na kuahidi kuwa hatagombea tena urais. Ameongoza Tunisia kwa miaka 23. Haijafahamika bado kama hotuba ya rais itatuliza ghasia ambazo maafisa wa Tunisia wanasema zimeacha watu 23 wamekufa. Makundi ya haki za binadamu na mashahidi wanasema idadi ya waliokufa iko juu zaidi.

XS
SM
MD
LG