Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 01:56

Kiongozi wa Seneti, Haiti ashambuliwa kwa risasi


Rais wa baraza la Seneti la Haiti, Joseph Lambert, amepigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili katika eneo moja la jiji la Port-au-Prince, karibu na jengo la bunge. 

Mwanafamilia mmoja aliiambia VOA kwamba Lambert anatibiwa majeraha yake katika hospitali moja katika mji mkuu wa Haiti.

Tukio hilo limetokea siku mbili kabla ya muda wa masharti ya kundi dogo la maseneta, viongozi pekee waliochaguliwa kwa sasa nchini Haiti kwisha.

Haiti inajitahidi kudhibiti ongezeko la ghasia za magenge na utekaji nyara ambao ulisababisha serikali mwezi uliopita kuomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa.

Serikali ya Waziri Mkuu Ariel Henry, inaliomba jeshi la haraka kuingilia kati nchini Haiti ili kusaidia kuzima ghasia za magenge.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili suala hilo, lakini hakuna uamuzi uliotolewa.

Mnamo Novemba 2022, Lambert alikuwa mmoja wa wanasiasa wawili wa Haiti waliolengwa na vikwazo vya wizara ya fedha ya Merika. Maafisa wa Marekani wanamshutumu Lambert kwa kujihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Canada pia iliweka vikwazo dhidi ya mwanasiasa huyo wa wa muda mrefu.

Seneta Lambert amekanusha madai hayo na kuapa kupambana na vikwazo hivyo vinavyo mkabili mahakamani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG