Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 21:10

Kiongozi wa Russia akiri Kyiv imepata 'mafanikio makubwa'


FILE -Rais wa Russia Vladimir Putin (Valeriy Sharifulin/TASS Host Photo Agency/Handout via Reuters)
FILE -Rais wa Russia Vladimir Putin (Valeriy Sharifulin/TASS Host Photo Agency/Handout via Reuters)

Ukraine imedai kupata ushindi mpya katika kujibu mashambulizi dhidi ya majeshi ya Russia Ijumaa wakati kiongozi aliyeteuliwa na Russia katika eneo la mashariki katika  mkoa wa Kharkiv akikiri kuwa Kyiv imepata “mafanikio makubwa.”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba ya kila siku usiku kwa njia ya video Ijumaa kuwa majeshi ya Ukraine yamekamata tena zaidi ya makazi 30 katika mkoa wa Kharkiv.

“Sisi tunaendelea polepole kuchukua udhibiti wa maeneo zaidi, na kurejesha bendera ya Ukraine na ulinzi wa watu wetu,” Zelenskyy alisema.

Mapema Jumamosi, kituo cha televisheni cha serikali ya Russia kilitangaza mahojiano na kiongozi aliyeteuliwa na Russia kuongoza Kharkiv, Vitaliy Hanchev, aliyesema, “hali ni mbaya sana hapa hivi sasa. Ukweli ni kwamba kulikuwa na ukiukaji wa ulinzi wetu jambo ambalo tayari ni ushindi tosha kwa majeshi ya Ukraine.”

Mafanikio ya Ukraine karibu na Kharkiv ni hatua ya haraka zaidi iliyoripotiwa na kila upande kwa miezi kadhaa, na ni moja ya mabadiliko makubwa sana katika kasi ya vita tangu majeshi ya Russia yalipokimbia mashambulizi yenye maafa makubwa katika mji mkuu, Kyiv, mwezi Machi.

Wachambuzi wa kivita wa Magharibi wanasema kupiga hatua huko kuna waweka Waukraine uwezo wa kushambulia njia kuu ya reli ambayo Moscow imekuwa ikiitegemea kwa ajili ya kupeleka mahitaji kwa majeshi yake upande wa mashariki mwa Ukraine na inaweza kuwaacha wanajeshi wa Russia katika hatari ya kukosa kabisa mawasiliano.

Taasisi ya tafakuri ya Utafiti wa Kivita imesema majeshi ya Ukraine yalikuwa ndani ya kilomita 15 kutoka Kupiansk, maungano ya njia ya reli ambayo Moscow imekuwa ikiitumia.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema katika taarifa zake za kipelelezi zilizobandikwa kwenye mtandao wa Twitter Jumamosi kwamba iwapo Ukraine itauteka mji wa Kupiansk “hilo litakuwa pigo kubwa Russia.”

Zelenskyy aliweka video mapema wiki hii inayowaonyesha wanajeshi wa Ukraine wakitangaza walikuwa wameuteka mji wa mashariki wa Balakliya, na eneo la mstari wa mbele la kusini mwa Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Majeshi ya Ukraine yalisema yamepiga hatua takriban kilomita 50 katika eneo la mstari wa mbele baada ya shambulizi lililoonekana limewashtukizia warussia.

Huko Prague, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amewaambia waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Czech, “Tunaona mafanikio huko Kherson hivi sasa, tunaona mafanikio huko Kharkiv, hivyo basi, hilo linatupa moyo sana, sana.”

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza alisema katika ripoti yake ya kipelelezi, “Wakati operesheni za Ukraine zikiwa zinaendelea huko Kherson, ulinzi wa Russia katika mstari wa mbele umepata shinikizo kutoka pande zote mbili kaskazini na kusini.”

XS
SM
MD
LG