Etake amesema watu wasiojulikana walimshambulia kwa kumtupia pilipili kali” Jumatatu usiku wakati akiondoka kwenye mgahawa kurejea nyumbani.
Washambuliaji hao, amesema katika mtandao wa Facebook, walikuwa katika gari ndogo na kukimbia mara moja baada ya kumtupia mkorogo wa pilipili katika uso wake.Etale alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani Jumanne majira ya saa saba na nusu.
Washambuliaji hao walimkabili wakati Etale akielekea katika gari lake lililokuwa limeegeshwa katika jengo la baada ya chakula cha usiku akiwa na marafiki zake katika mgahawa wa Ronalo Foods ulioko Mtaa wa Kimathi katikati ya jiji la Nairobi. Nilikuwa nimefuatana na rafiki yangu Phelix G-cord na baadae tuliungana na rafiki zetu wengine, Onyango Kevin na pia alishiriki na sisi baadaye rafiki ya kipenzi wa zamani Oliver Mugo, ameandika "Nilikuwa katika hali ya furaha na marafiki zangu na nikaamua kuondoka kwenda nyumbani mida ya saa nne na dakika kumi usiku ilikupumzika kwa ajili ya kujiandaa na shughuli za siku ya pil. Nilianza kutembea kuelekea CFC Stanbic Bank pole ili niweze kumfikia Phelix ambaye alikuwa tayari amevuka barabarani."
Wakati akiwa katikati ya barabara, gari dogo lilipita na nikasimama kulisubiri. Lakini sikuweza kuona idadi ya watu waliokuwa ndani ya gari. Kwa ghafla, katika kipindi kifupi, baadhi ya watu hao walishuka, wakamtupia mkorogo mzito kwenye uso wake na ukaelekea kwenye macho na gari likaondoka kuelekea kwenye kituo cha petrol upande wa Mtaa wa Kimathi, amesema.;Etale amesema kuwa anabahati kuwa bado yuko hai.
Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Robinson Thuku amesema kuwa mpaka saa tatu na nusu asubuhi Jumanne walikuwa hawajapokea repoti yoyote au malalamiko kutoka kwa Etale ilikusaidia katika upelelezi