Kiongozi wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema leo kwamba sitisho la mapigano la takriban miezi miwili nchini Syria bado linakabiliwa na matatizo lakini inatoa nafasi muafaka ya kuleta mabadiliko ya Amani kwenye mzozo unaondelea.
Sitisho la mapigano lilianza kutekelezwa mwezi Februari kati ya vikosi vinavyoungwa mkono na serikali na vile vya wapiganaji kutoka upinzani ambalo limesifiwa kwa kupunguza mapigano nchini Syria.
Hata hivyo pande zote zimeripoti ukiukaji mkubwa wa mkataba huo pamoja na ongezeko la mapigano katika kipindi cha wiki chache zilizopita. Stoltenberg ameyasema hayo kwenye kikao na waandishi wa habari kwenye taarifa ya pamoja akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, mjini Ankara.