Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 12:32

Diplomasia ya Korea Kaskazini yamfikia Rais wa Korea Kusini


Mualiko wa kipekee kutoka Pyongyang kwa Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ulikuwa umetolewa siku ya pili na utawala wa Kim Jong-un wakati wawakilishi wake wakitembelea  barabara maarufu ya Kim dynasty ya Kusini Jumamosi.

Hiyo ni sehemu ya muendelezo wa maelewano ya kidiplomasia ambayo yalihusisha kupeana zaidi mikono, kujiburudisha na baadhi ya vinywaji vya Korea wakati wa chakula cha mchana na furaha ya pamoja ya kuangalia timu "zilizoungana" za Korea zikicheza mchezo wa hockey wakati wa michezo ya Olympic ikiwa katika siku ya pili huko Korea Kusini.

Hakuna kilichoamuliwa na Rais wa Korea Kusini kuhusu mualiko huo lakini iwapo utafanyika itakuwa ni wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi baina ya nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Moon amesisitiza umuhimu wa kuwepo mkutano huo na ameeleza hatua hiyo ya Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo na Marekani.

Ujumbe huo wa mdomo uliotolewa kwa "wakati unaostahili" kutoka kwa dikteta Kim Jong Un, uliwasilishwa na dada mdogo wa Kim Yo Jong, ni sehemu ya hatua za haraka za kuboresha hisia kati ya pande mbili zenye mvutano wakati wa michezo ya Olympic ya Pyeongchang.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG