Traore ambaye alikuwa ameahidi kurejesha utawala wa kidemokrasia kupitia uchaguzi ifikapo Julai 2024, alitangaza pia mipango ya mabadiliko kwenye katiba ya nchi ikizingatia zaidi matakwa ya wananchi,
“Sio kipaumbele, nawambia hilo wazi, usalama ndio kipaumbele” katika nchi iliyokumbwa na ghasia za wanajihadi, aliwambia waandishi wa habari akizungumzia suala la uchaguzi.
Hata hivyo, lengo lilikuwa kuandaa uchaguzi, alisema, bila kutangaza lini uchaguzi utafanyika.
Traore alisema “Hakutakuwa uchaguzi utakaojikita tu Ouagadougou na Bobo-Dioulasso na miji mingine ya karibu,” akimaanisha miji miwili ambayo haikukumbwa kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajihadi.
Forum