Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:28

Kiongozi wa kijasusi Uingereza ashuku azma ya Iran kusitisha program ya nyuklia


Mkuu wa idara ya ujasusi Uingereza Richard Moore 2
Mkuu wa idara ya ujasusi Uingereza Richard Moore 2

Kiongozi wa idara ya  ujasusi ya Uingereza Richard Moore, amesema Alhamisi kwamba haamini kwamba kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ana azma ya kufufua mkataba wa nyuklia na  mataifa yenye nguvu duniani, licha ya kuendelea na mazungumzo.

Moore anayeongoza idara hiyo maarufu kama SIS au M16, amesema kwamba anaamini kufufuliwa kwa mkataba wa 2015 maarufu kama JCPOA, ndiyo njia bora zaidi ya kudhibiti program ya nyuklia ya Iran. Chini ya mkataba huo, Iran ilikuwa imekubali kupunguza uzalishaji wake wa nyuklia ili kuondolewa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi na mataifa hayo.

Tangu rais wa Marekani aliyeondoka madarakani Donald Trump kuiondoa Marekani kwenye mkataba huo 2018, Iran imekiuka masharti mengi yaliyowekwa, wakati ikiendelea kusindika uranium yenye viwango vya kutengeneza silaha. Mataifa ya magharibi yameonya kwamba Iran inakaribia kutengeneza bomu la nyuklia , suala ambalo imekanusha vikali.

XS
SM
MD
LG