Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:30

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Zimbabwe ajiuzulu kwenye uongozi wa chama


Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa Alhamisi ametangaza kujiuzulu kwenye uongozi wa chama miezi michache baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais, akilaani “vitisho na vurugu” zinazofanywa na utawala.

“Hii ni kuwatangazia rasmi raia wenzangu wa Zimbabwe na dunia nzima, kwamba kuanzia sasa, sina uhusiano wowote tena na chama cha CCC,” Chamisa amesema katika taarifa.

Amekishtumu chama tawala cha ZANU PF cha Rais Emmerson Mnangagwa kutumia vyombo vya dola kukidhoofisha chama cha CCC.

Uamuzi huo wa kushangaza unajiri baada ya Mnangangwa, mwenye umri wa miaka 81 kushinda muhula wa pili, kwa kumshinda kiongozi huyo wa chama cha the Citizens Coalition for Change(CCC), katika uchaguzi ambao ulikipa chama tawala cha ZANU-PF wingi wa viti katika bunge.

Waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi haukukidhi vigezo vya demokrasia na mvutano wa kisiasa uliongezeka tangu wakati huo.

Forum

XS
SM
MD
LG