Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:56

Kiongozi wa chama cha upinzani akamatwa Uganda kwa kudai maendeleo


Polisi wa Uganda
Polisi wa Uganda

Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda na makundi ya kutetea haki za kibinadamu wanataka maafisa wa usalama kumuachilia huru mwanasiasa wa upinzani Joseph Kabuleta aliyekamatwa Juamatatu.

Polisi wanadai kwamba Kabuleta, ambaye ni rais wa chama cha National economic Empowerment Dialogue NEED, amekuwa akieneza ujumbe wenye ubaguzi kwa msingi wa makabila.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu hata hivyo yanashutumu maafisa wa usalama kwa kukandamiza wakosoaji wa serikali.

Kabuleeta amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa serikali, ikiwemo kile amekuwa akitaja kama huduma mbovu za serikali katika sehemu mbali mbali za Uganda.

Wakili wa Kabuleta Ivan Bwowe, ameambia VOA kwamba ilichukua siku nzima kwa polisi kusema mahali ambapo walikuwa wanamzuilia.

Polisi wanasema kwamba madai ya Kabuleta kwamba baadhi ya sehemu za nchi zinapokea maendeleo kutoka kwa serikali kuliko zingine, yanaweza kusababisha chuki kati ya raia wa Uganda.

XS
SM
MD
LG