Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:49

Kiongozi wa Al-Shabab auwawa


Wanamgambo wa Al-Shabab wa Somalia
Wanamgambo wa Al-Shabab wa Somalia

Somalia imesema ndege ya Marekani, isiyo na rubani “drone” imefanya mashambulizi siku ya Jumamosi na kumuua kiongozi wa juu wa wanamgambo wa Al-Shabab, Yusuf Dhee.

Serikali imesema katika taarifa yake Jumatano kwamba Dheeg, alilengwa na shambulizi hilo na alikufa pamoja na makamanda wengine wa Al-Shabab mjini Dinsor.

Chanzo kutoka kwa wanamgambo kimeithibitishia Sauti ya Amerika kifo hicho kusini mwa mji huo.

Serikali ya Somalia inasema Dheeg, ambaye alikuwa mkuu wa mambo ya nje wa Al-Shabab, alihusika katika mashambulizi ya ndani na nje ya Somalia.

Kiongozi huyo alikuwa mpangaji mkuu wa mashambulizi ya Al-Shabab.

XS
SM
MD
LG