Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:15

Kiongozi mwingine wa cheo cha juu Sudan ajiuzulu


Aisha Musa Sayyed akisalimiana na wanamichezo huko Khartoum, Sudan.
Aisha Musa Sayyed akisalimiana na wanamichezo huko Khartoum, Sudan.

Aisha Musa Sayeed, aliwashutumu viongozi wa kijeshi kwa kuwaweka kando raia na kufanya maamuzi ya upande mmoja yanayoathiri nchi nzima ikijumuisha matumizi ya nguvu ya hivi karibuni dhidi ya waandamanaji wa amani

Mwanachama raia wa Baraza kuu la utawala la Sudan amejiuzulu akielezea kutokana na kuingiliwa kati kwa kazi yake na maafisa wa jeshi katika serikali ya mpito.

Aisha Musa Sayeed, aliwashutumu viongozi wa kijeshi kwa kuwaweka kando raia na kufanya maamuzi ya upande mmoja yanayoathiri nchi nzima ikijumuisha matumizi ya nguvu ya hivi karibuni dhidi ya waandamanaji wa amani.

Sayeed aliwaambia waandishi wa Habari kwenye mkutano wa mwishoni mwa wiki mjini Khartoum kwamba aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa sababu upande wa jeshi katika baraza la utawala ulipuuza maoni ya wanachama wengine wa baraza. Sayeed ni raia wa tatu mwenye cheo cha juu nchini Sudan kuondoka kwenye wadhifa wake katika muda wa wiki moja.

Wiki iliyopita, mwanasheria mkuu wa Sudan, Taj Al Sir Al Hibir, alijiuzulu akieleza kuingiliwa katiak kazi zake kutoka idara zisizoidhinishwa na serikali, katika ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma, ambapo aliita ni ukiukaji wa wazi wa sheria.

Pia jaji mkuu, Neimat Abdallah Mohammed Khair, jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo aliondolewa kutoka katika wadhifa wake wiki iliyopita na baraza kuu bila kutoa maelezo.

XS
SM
MD
LG