Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:30

Kiongozi mkuu wa upinzani Senegal Ousmane Sonko afunguliwa mashtaka mapya na chama chake kimefutwa


Kiongozi w upiunzani Senegal Ousmane Sonko alipozungumza na waandishi wa habari Mach 8, 2021 baada ya kutolka kizuizini.

Waziri wa mambo ya ndani atangaza chama cha Sonko Pastef Les Patriotes kimefutwa

Raia wa Senegal waliachwa na mshangao siku ya Jumanne, siku moja baada ya kiongozi mkuu wa upinzani Ousmane Sonko kufunguliwa mashtaka mapya na chama chake kuvunjwa na kuharibu mipango yake ya kugombea urais.

Mwanasiasa mwenye umaarufu na mkosoaji mkuu wa Rais Macky Sall, ambaye ni maarufu sana miongoni mwa vijana amekabiliwa na msururu wa matatizo ya kisheria anayodai yanalenga kumweka nje ya siasa.

Nimekasirishwa nilitoka jana na kwenda kuandamana lakini kulikuwa hakuna mtu yeyote nje, alisema Thierno Mbaye, mfuasi wa Sonko aliyehojiwa na AFP katika mji mkuu wa Dakar. Sina matumaini tena aliongeza.

Siku ya Jumatatu Sonko alishtakiwa kwa kuchochea uasi, kudhoofisha usalama wa serikali, ushirikiano wa uhalifu na kundi la kigaidi na uhalifu mwingine.

Chini ya saa mbili baadaye waziri wa mambo ya ndani alitangaza chama chake cha PASTEF kingevunjwa.

Vyama vya siasa ni nadra kufutwa nchini Senegal. Mara ya mwisho ilifanyika mwaka 1966 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Forum

XS
SM
MD
LG