Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:06

Kingunge aweka bayana kilichofanyika ndani ya CCM huko Dodoma


Wagombea watatu bora wa urais kupitia CCM mwaka 2015
Wagombea watatu bora wa urais kupitia CCM mwaka 2015

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania bwana Kingunge Ngombale Mwiru alibainisha kwamba mchakato wa kumpata mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao haukwenda vizuri huku kukiwa na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za chama.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bwana kingunge ambaye alikuwa akimuunga mkono mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo ya urais kupitia chama tawala cha CCM, Bwana Edward Lowassa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam hapo Jumatano kuwa mchakato wa kupata wagombea unatakiwa kuanzia kamati kuu kama ilivyofanyika miaka ya nyuma na wagombea wote yaani mmoja mmoja kupita kwenye kamati kuu na kupewa nafasi ya kujieleza jambo ambalo halikufanyika katika mchakato uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma ambapo kamati kuu ilipokea tu majina matano kutoka kamati ya maadili ambayo haina madaraka hayo.

Kingunge Ngombale Mwiru
Kingunge Ngombale Mwiru

Aidha alisema ukiukwaji huo wa utaratibu wa kawaida wa kumpata mgombea katika chama cha CCM unaweza kutafsiriwa kwamba kulikuwa kuna kikundi cha watu chenye maslahi binafsi ya kumpata mgombea waliyempanga na kutaka kamati kuu ipokee hivyo hivyo jambo ambalo ni dharau kwa wagombea wote waliojitokeza na ni dharau kwa chama pia.

Hata hivyo alionyesha dhamira ya kutaka chama kifanye utaratibu wa kupata maridhiano na makundi ambayo hayakuridhika na mchakato huo ili kujenga umoja ndani ya chama na kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na ukweli kwamba bwana Lowassa bado anaungwa mkono na mamilioni ya watanzania.

Alipoulizwa juu ya uvumi kwamba anafikiria kujiondoa ndani ya chama cha CCM bwana Kingunge hakutaka kuweka bayana azma hiyo licha ya kusema kwamba wakati ukifika yeye binafisi kama anataka kuhama chama atatoa taarifa.

John Magufuli
John Magufuli

Katika mchakato huo uliofanyika mjini Dodoma siku chache zilizopita Dr.John Pombe Magufuli alichaguliwa kubeba bendera ya Chama Cha Mapinduzi-CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

XS
SM
MD
LG