Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:56

Kimbunga chatarajiwa pwani ya Marekani


Athari za upepo mkali katika mji wa Washington, Machi 2, 2018.

Wakaazi wa maeneo ya kusini mwa pwani ya Marekani wanakabiliana na kimbunga kikubwa kinachojulikana kama Nor’easter kinachotabiriwa kitasababisha upepo mkali, barafu na mvua nzito nchini.

Pia utabiri wa hali ya hewa unasema kuwa huenda kimbunga hicho kitaleta mafuriko makubwa katika pwani zote za eneo hilo kutoka mji wa Maine hadi Jimbo la North Carolina.

Ofisi za serikali ya Washington zimefungwa Ijumaa, kutokana na kimbunga hicho.

Hali kadhalika mvua nzito zinatarajiwa katika maeneo ya pwani ya New Jersey na upande wa mashariki wa Massachussets na mafuriko yanatabiriwa kuendelea hadi siku ya jumapili katika maeneo ya jimbo la Rhode Island.

Idhara ya utabiri wa hali ya hewa imeonya kwamba huenda kimbunga hicho kikasababisha matatizo ya usafiri katika baadhi ya maeneo ya Marekani.

Barafu nzito inatarajiwa kuanguka katika maeneo ya magharibi mwa jimbo la New York na kaskazini mwa Pennsylvania na huenda barafu hiyo ikafikia sentimita 20 au 30 kwa ukubwa.

Maafisa wa uokoaji wapo tayari kukabiliana na athari zozote zitakazojitokeza.

XS
SM
MD
LG