Polisi wamesema kwamba watu watano wamefariki kutokana na kimbunga hicho na kwamba huenda idadi ikaongezeka.
Onyo hilo limetokea huku shughuli za uokoaji zikiendelea, huku baadhi ya watu wakiwa hawajulikani walipo baada ya kimbunga kutokea siku tatu zilizopita.
Shughuli za uokoaji zinaendelea.
Kimbunga Gabrielle kimesababisha uharibifu mkubwa ambao haujawahi kuonekana nchini New Zealand kwa miongo kadhaa.
Hali ya dharura ilitangazwa Jumanne, na kuruhusu serikali kutoa msaada zaidi kwa watu katika sehemu zilizoathirika.