Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:17

Kimbunga Irene chapiga Marekani


Mawimbi yaliyosababishwa na kimbunga Irene yakipiga katika Virginia Beach , Virginia., Jumamosi, Aug. 27, 2011.
Mawimbi yaliyosababishwa na kimbunga Irene yakipiga katika Virginia Beach , Virginia., Jumamosi, Aug. 27, 2011.

Kimbunga Irene kimefika nchi kavu kikiwa na kasi ya kilomita 140 kwa saa

Kimbunga Irene kimepiga nchi kavu mashariki ya Marekani katika jimbo la North Carolina mapema Jumamosi, na kuanza kupanda kuekelea mwambao mzima wa mashariki ya nchi.

Kimbunga hicho kimefika nchi kavu kikiwa na kasi ya kilomita 140 kwa saa na kuteremsha mvua kali katika mwambao wa mashariki. Katika jimbo la North Carolina kimbunga hicho tayari kimeangusha miti, kusababisha mafuriko katika mitaa ya miji na kukosesha umeme maelfu ya watu.

Watabiri wa hali ya hewa katika kituo cha taifa kinachofuatilia vimbunga walishusha ubashiri wa ukali wa kimbunga hicho majira ya asubuhi mapema Jumamosi. Lakini bado wanatahadharisha kuwa kimbunga hicho ni hatari katika eneo zima la mashariki kuanzia Washington hadi New york ambalo lina wakazi wengi.

Ilani ya kimbunga imetolewa kwa ajili ya New York na sehemu kubwa ya mashariki katika kile ambacho Rais Barack Obama amesema ni dhoruba "ya hatari na itakayosababisha hasara kubwa"

Mashirika ya ndege tayari yamefuta mamia ya safari za ndege kwingineko mashariki mwa Marekani, na huduma za magari moshi katika baadhi ya maeneo pia zimefutwa.

Kimbunga cha Irene ni dhoruba ya kwanza kutishia vibaya eneo la mashariki mwa Marekani katika muda wa miaka mitatu iliyopita. Tayari kimeuwa mtu mmoja Puerto Rico na wengine wawili katika Jamhuri ya Dominican, na pia kusababisha uharibifu wa nyumba katika visiwa vya Bahamas.

XS
SM
MD
LG