Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 14:00

Kimbunga Batsirai chasababisha madhara Madagascar


Watu walioathiriwa na kimbunga Batsirai wakiwa katika kituo cha kuwahifadhi nchini Madagascar.

Kimbunga Batsirai kimeuwa watu takriban 10 na kukosesha makazi wengine 48,000 wakati kilipopiga Madagascar usiku kucha, shirika la udhibiti wa majanga limesema Jumapili.

Kimbunga hicho baadaye kilipungua nguvu lakini sio kabla ya kusababisha uharibifu katika taifa hilo masikini la kisiwa cha Bahari ya Hindi ambalo bado linajaribu kuondoka na Dhoruba mbaya ya kitropiki iliyopiga mapema mwaka huu.

Baadhi ya maeneo yalikabiliwa na mvua kubwa na upepo kabla ya kimbunga kutua huko Mananjary.

Shirika la Habari la AFP limeshuhudia kimbunga hicho kikiwa kimeng’oa miti na kuharibu majengo.

Wakati huohuo, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani - WFP linanukuu makadirio kutoka kwa maafisa wa ndani kwamba watu takriban 595,000 wanawaza kuwa wameathiriwa moja kwa moja na kimbunga Batsirai.

Pia wengine 150,000 wanaweza kuwa wamekoseshwa makazi kwa sababu ya maporomoko mapya ya ardhi na mafuriko.

Hali hiyo ya dhoruba imehatarisha maisha ya karibu watu milioni 4.4 kwa ujumla, shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Mwezi mwekundu yamesema.

XS
SM
MD
LG