Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 18:27

Kimbunga Alfred chapunguza kasi Australia


Kimbunga Alfred kilidhoofika kitropiki Jumamosi kilipokaribia kuwa mvua na upepo uliovuma pwani ya mashariki mwa Australia ambapo mamia ya maelfu ya nyumba hazikuwa na umeme.

Kimbunga cha zamani cha kitropiki kiko umbali wa kilomita 65 kutoka pwani ya mji mkuu wa Queensland Brisbane, watabiri wa serikali wamesema katika sasisho la mwisho.

Ingawa sasa bila upepo mkali, dhoruba hiyo ilikwenda polepole uelekeo wa pwani na kusababisha mvua kubwa kabla ya kutarajiwa kuvuka bara baadaye mchana.

“Licha ya kudhoofika kwake, mvua kubwa huenda ikaendelea kunyesha kusini mashariki mwa Queensland na kaskazini mashariki mwa New South Wales mwishoni mwa juma,” ofisi ya utabiri wa hali ya hewa imesema.

Mvua hizo bado zinaweza kusababisha mafuriko makubwa na kutishia maisha kwenye eneo la kilomita 400 la ukanda wa pwani unaozunguka majimbo hayo mawili.

Forum

XS
SM
MD
LG