Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 13:40

Kim Jong Un ameamuru wanajeshi kupambana na Corona


Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un akiongoza mkutano kuhusu COVID-19 mjini Pyongyang, Korea kaskazini, May 17, 2022.

Korea kaskazini imetangaza kwamba inatumia madaktari wa jeshi lake katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona mjini Pyongyang.

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un ameamuru wanajeshi wa taifa hilo kukabiliana na janga hilo baada ya maambukizi mengi kuripotiwa tangu wiki iliyopita.

Visa 232,880 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimeripotiwa, huku watu sita wakifariki kufikia leo jumanne.

Jumla ya watu 691,170 wametengwa kwa uchunguzi kubaini iwapo wameambukizwa corona.

Watu 62 wamefariki tangu mwezi April, huku watu milioni 1.7 wakionyesha dalili za kuambukizwa Corona nchini Korea kaskazini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG