Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 03:46

Kikwete na Kenyatta wazungumza Ikulu Nairobi


Rais Jakaya Kikwete na Uhuru Kenyatta katika mkutano mapema mwaka huu.
Rais Jakaya Kikwete na Uhuru Kenyatta katika mkutano mapema mwaka huu.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania leo amefanya mazungumzo na Rais Kenyatta wa Kenya katika Ikulu ya Nairobi,siku moja kabla ya kuhutubia mabaraza mawili ya bunge la Kenya mjini Nairobi.

Rais Kikwete aliwasili nchini Kenya jana jumapili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania. Punde baada ya kuwasili katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi, Rais Kikwete alipokelewa kwa heshima kamili za jeshi la nchi kavu kabla ya kukagua gwaride ya heshima.Alipigiwa mizinga 21 kabla ya wimbo wa taifa wa Tanzania na mazungumzo na Rais Kenyatta.

Kikwete na Kenyatta wafanya mazungumzo
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:45 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akiwa na Rais Kenyatta kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania,viongozi hao wawili walikagua ujenzi wa barabara mpya inayojengwa kuunganisha nchi hizi mbili kwa urahisi zaidi.

Barabara hiyo ya kilomita 90 itaunganisha sehemu za Taveta na Mwatate nchini Kenya na mji wa Arusha na Holili.
Kwenye tukio hilo, Rais Kenyatta alisema watu wa nchi hizo mbili wamekuwa kitu kimoja tangu zamani licha ya mipaka inayo-watenganisha.

Kabla ya kuondoka hapa nchini Rais Kikwete atahutubia mabaraza mawili ya Bunge la Kenya na kufafanua zaidi kuhusu ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania na hususan maswala nyeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG