Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:57

Kikwete:Baadhi ya viongozi wa Afrika wanatumiwa na mataifa ya nje


Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika-AU, umefanyika Jijini Dar es salaam nchini Tanzania Jumatatu ambapo suala la migogoro katika baadhi ya nchi za Afrika limejadiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo wa AU Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alitoa tahadhari kwa baadhi ya viongozi barani Afrika ambao amedai wanatumiwa na watu wa mataifa ya nje kuchochea migogoro katika bara hili

Bila kutaja majina yao Rais Kikwete alisema zama hizo za kutumiwa zimeanza kutoka wakati wa ukoloni mpaka hivi sasa.

Rais Kikwete alielezea chanzo cha migogoro barani Afrika ni kwamba ukoloni uliokuwa unawagawa waafrika ili uwatawale na pia mipaka ambayo mingi iliwekwa kwa maslahi ya watawala.

Aidha Rais Kikwete, alisifia juhudi za Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na vyombo vyake katika kufanikisha kutatua matatizo yanayozikabili nchi mbalimbali barani humo ambapo alisema kwa sasa migogogoro mingi imepungua ikiwemo mgogoro wa hivi sasa nchini Madagascar.

Mkutano huo wa 368 wa baraza la amani na usalama la AU unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe na kuhudhuriwa pia na rais mstaafu wa Msumbiji na mpatanishi mkuu wa mgogoro wa Madagascar Joachim Chisano.
XS
SM
MD
LG