Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:54

Kikosi cha nchi nne za Afrika magharibi kinasema kimewaua wanamgambo wa kiislamu 805


Picha ya angani inaonyesha kijiji cha Ngouboua nchini Chad baada ya kijiji hicho kushambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram, February 13, 2015. Picha ya Reuters
Picha ya angani inaonyesha kijiji cha Ngouboua nchini Chad baada ya kijiji hicho kushambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram, February 13, 2015. Picha ya Reuters

Kikosi cha kimataifa kinachojumuisha wanajeshi kutoka Nigeria, Niger, Cameroon na Chad Jumanne kimesema kiliua zaidi ya wanamgambo wa kiislamu 800 katika kipindi cha miezi miwili katika eneo lenye usalama mdogo la ziwa Chad.

Nchi hizo nne za Afrika magharibi pamoja na Benin ziliunda kikosi hicho mwaka wa 2015 kupambana na kundi la Boko Haram na hasimu wake, the Islamic State in West Africa Province ( ISWAP).

Kikosi kazi hicho cha mseto (MNJTF) kimesema wanamgambo wa kiislamu 805 waliuawa kwenye visiwa vya ziwa Chad na maeneo jirani kati ya tarehe 28 Machi na tarehe 4 Juni, wakiitaja operesheni hiyo kuwa yenye maafanikio.

Bonde kubwa la Ziwa Chad linavuka mipaka ya Nigeria, Niger, Cameroon na Chad, Boko Haram na ISWAP waliweka ngome zao kwenye visiwa vyake vingi vidogo.

Takriban wanajeshi 3,000 kutoka nchi hizo nne walihusika katika opereheni hiyo na kuteka au kuharibu magari 44, pikipiki 22 na silaha, uwanjani, kwenye bahari na katika operesheni za anga, kikosi hicho kimesema.

Risasi zilikamatwa na vituo vya kutengeneza vilipuzi vilivyoboreshwa viliharibiwa, kikosi hicho kimesema.

Kikosi hicho kimeongeza kuwa wanajeshi 20 kutoka Niger walijeruhiwa, na mmoja yuko katika hali mbaya.

XS
SM
MD
LG