Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:19

Kikosi cha kupambana na rushwa FIFA kwenda Zimbabwe


Rais wa FIFA Joseph Blatter .

Kikosi cha kupambana na rushwa FIFA kwenda Zimbabwe kukamilisha uchunguzi wa madai ya rushwa kwa timu ya taifa nchini humo.

Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu duniani (FIFA) litakwenda Zimbabwe wiki ijayo ili kukamilisha uchunguzi wake juu ya shutuma kwamba wachezaji wa nchi hiyo walichukua rushwa ili kushindwa katika mashindano.

Rais wa Shirikisho la soka la Zimbabwe Ndumiso Gumede alisema leo kuwa mkuu wa usalama wa FIFA Chris Eaton ataongoza timu ya kupambana na rushwa.

FIFA inategemewa kuitoza faini au pengine kuwafungia maisha wachezaji kadhaa wa Zimbabwe.

Shirikisho la soka Zimbabwe ZIFA limesema lina ushahidi kuwa wachezaji wake walipokea malipo ili kupoteza michezo wakati wa mechi za kimataifa huko Asia miaka ya nyuma kufikia 2007.

XS
SM
MD
LG