Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:28

Kikao cha bunge la Marekani kuanza Jumanne


Kikao cha 118 cha Bunge la Marekani kinafunguliwa rasmi Jumanne na matarajio yakiwa mengi.

Jambo kubwa linalotupiwa macho zaidi ni iwapo mwakilishi Kevin McCarthy, wa California anaweza kupata kura za kutosha za Warepublikan wenzake ili kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi.

McCarthy, mwenye umri wa miaka 57, kwa miaka mingi amekuwa akitaka kuongoza baraza hilo lenye wajumbe 435.

Warepublican walipata ushindi mdogo wa viti 222 dhidi ya 213 katika uchaguzi wa katikati ya awamu mwezi Novemba.

Kwa ushindi huyo watachukua na udhibiti wa bunge kutoka kwa Wademokrat na kuchukua uspika wa bunge kutoka kwa Nancy Pelosi anayemaliza muda wake.

Wademokrat, ambao wamekuwa katika mgawanyiko wa 50 kwa 50 na Republikan katika Seneti miaka miwili iliyopita, walipata upinzani katika uchaguzi uliopita.

XS
SM
MD
LG