Polisi wa London wanasema mapema Alhamisi hawajapata ushahidi wowote wa kuashiria msimamo mkali unaoashiria ugaidi kwa kijana wa Kisomali.
Kijana huyo alichunguzwa baada ya kumjeruhi mwanamke mmoja na kusababisha kifo chake na kujeruhi wengine watano katikati ya jiji la London.
Badala yake polisi wanasema tukio hilo kuna uwezekano limesababishwa na matatizo ya akili.
Polisi imemkamata kijana mwenye umri wa miaka 19 katika eneo la Russel Square, karibu na chuo kikuu cha London, baada ya kukabiliana nae na vifaa vya umeme.
Kijana huyo ambaye wajihi wake bado haujatangazwa kwa umma kwa sasa yupo mikononi mwa polisi katika hospitali moja ya huko.