Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 04:43

Kiir: Nitawania tena urais wa Sudan Kusini


Rais wa Sudan, Salva Kiir.
Rais wa Sudan, Salva Kiir.

Kiongozi wa Sudan Kusini, Salva Kiir, Jumanne aliahidi kwamba uchaguzi uliocheleweshwa, utafanyika mwaka ujao kama ilivyopangwa, na kwamba atawania urais.

Kiir, kamanda mkuu wa wapiganaji wa msituni, amekuwa rais pekee wa taifa hilo tangu alipoliongoza kupata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011.

Taifa hilo limeshuhudia migogoro ya mara kwa mara wakati wa uongozi wa Kiir, na linashikiliwa pamoja na serikali dhaifu ya umoja, chini ya uongozi wa Kiir na Makamu wake, Riek Machar. Kipindi cha mpito kilitarajiwa kuhitimishwa kwa kufanyika uchaguzi, mwezi Februari mwaka huu, lakini serikali hadi sasa imeshindwa kufikia makubaliano muhimu, ikiwa ni pamoja na maafikiano ya kuandaa rasimu ya katiba.

"Ninakaribisha uidhinishaji wa kugombea urais mwaka 2024," Kiir aliwaambia wafuasi wa chama chake tawala cha Sudan People's Liberation Movement, akilielezea kama "tukio la kihistoria."

"Tumejitolea kutekeleza sura za mkataba wa amani kama ilivyoelezwa, na uchaguzi utafanyika mwaka wa 2024."

Hakuna mwanasiasa mwingine ambaye ametangaza nia yake ya kugombea, lakini hasimu wake wa muda mrefu, Riek Machar, anatarajiwa kugombea.

Forum

XS
SM
MD
LG