Kundi moja la kutetea haki za kibinadamu lilisema siku ya Jumatatu kuwa limepata ushahidi kwamba baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa nchini Sudan Kusini wamekuwa wakijifaidisha kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimekuwa vikiendelea katika nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na viongozi wa pande zinazopigana.
Waasisi wa kundi hilo, mcheza filamu wa Hollywood, George Clooney na mwanaharakati John Prendergast, walielezea wazi maoni yao wakati wa kikao na waandishi wa habari katika klabu cha kitaifa cha wanahabari mjini Washington.
Ripoti ya kundi hilo ambayo imepewa jina la sentry imewashutumu rais wa Sudan, Salva Kiir, makamu wa rais wa kwanza, Riek Machar, na majenerali wa Sudan Kusini, kwa kuiba mamilioni ya dola kutoka hazina ya taifa tangu mwaka wa 2005 wakati makubaliano ya amani yalipoafikiwa na kupelekea uhuru wan chi hiyo.