Mwili wa Cherubin Okende, mwenye umri wa miaka 61, waziri wa zamani wa uchukuzi, ulipatikana ukiwa umechanwa kwa risasi ndani ya gari lake tarehe 13 Julai kwenye barabara moja mjini Kinshasa baada ya kutoweka alipokuwa akielekea kuripoti kwenye mahakama ya katiba.
Uchunguzi wa maiti umeonyesha Okende “alifariki kutokana na kuvuja damu kutokana na kidonda kilichosababishwa na silaha aliyotumia mwenyewe”, mwendesha mashtaka Edmond Isofa aliwambia waandishi wa habari Alhamisi.
Msemaji wa chama chama cha Moise Katumbi cha EPR, Herve Diakiese ameiambia AFP kwamba amekasirishwa na “kunyimwa haki” na kumtaka mwendesha mashtaka “kuweka ripoti hiyo ya uchunguzi wa maiti hadharani.”
Vuguvugu linalotetea demokrasia la “Lucha” lilisema pia kwamba matokeo ya uchunguzi wa mahakama ni ya “kuudhunisha na ya upuzi kabisa”.
Waziri huyo wa zamani wa uchukuzi alijiuzulu kwenye serikali ya Rais Felix Tshisekedi na kujiunga na chama cha kiongozi wa upinzani Moise Katumbi, cha Together for the Republic (EPR).
Forum