Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imetoa onyo kwa makundi yanayopigania kujitenga kwa jimbo la pwani kutoka taifa la Kenya akihutubia kikao cha bunge mjini Nairobi kwa mara ya kwanza tangu kuidhinishwa katiba mpya rais Mwai Kibaki amesema serikali haitakubali kujitenga kwa jimbo la Pwani kutoka taifa la Kenya.
Rais huyo amesema jimbo la Pwani ni ardhi ya Kenya na jimbo hilo halitakubaliwa kujitenga. amesema Kenya ni taifa moja juhudi zozote za kulihgawanya taifa hilo zitakataliwa.
Katika muda wa majuma kadhaa yaliyopita suala hili limekuwa kwenye vyombo vya habari huku baadhi ya wakazi wa pwani wakisema hawatashiriki katika uchaguzi mkuu ujao kwasababu ya kutaka kujitenga na Kenya.
Vijana wafuasi wa kundi la Mombasa la Republikan Council wanadai wamekuwa wakibaguliwa na serikali katika sekta zote za kiuchumi na nia yao ni kujitenga na taifa la Kenya wanadai kwamba jimbo la Pwani liliunganishwa na nchi ya Kenya wakati wa uhuru.
Na viongozi wengi katika mkoa wa Pwani wanawaunga mkono vijana hao wakisema madai yao ni halali na imemlazimu waziri mkuu Raila Odinga kuwasihi vijana hao kuachana na dhana hiyo kama hatua ya kuilazimisha serikali kusikiliza matakwa yao .
Lakini mpaka hivi sasa vijana na wakazi wengi wa jimbo la Pwani bado wanalilia kujitenga na Kenya