Bunge la Sudan limetangaza kuwa Sudan Kusini ni adui kati kati ya ghasia zinazosambaa kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.
Baada ya upigaji kura mjini Khartoum jumatatu, waziri wa habari wa Sudan Kusini Barnaba Marial aliupinga uamuzi huo na kusema nchi yake si adui wa Sudan.
Rabi Abdelati Obeid mwanachama maarufu wa chama kinachotawala Sudan cha National Congress aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hali kati ya nchi hizo mbili hivi sasa ni hali ya kivita.
Alisema Sudan Kusini haiheshimu mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini.