Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:39

Khartoum na Juba zaendelea kushutumiana


Rais wa Sudan Omar al-Bashir (L) mwenye nguo nyeupe na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (R) mwenye suti nyeusi
Rais wa Sudan Omar al-Bashir (L) mwenye nguo nyeupe na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (R) mwenye suti nyeusi

Rais Thabo Mbeki amethibitisha kuwa kamati ya uangalizi inatarajiwa kukutana Alhamis

Mjumbe mkuu wa Sudan Kusini katika mazungumzo na Sudan anaishutumu Khartoum kuwa ina nia mbaya wakati nchi hizi mbili zikikaa chini kwa mazungumzo ya moja kwa moja juu ya masuala ya usalama.

Hali ya kutokuaminiana imeenea kwenye hoteli ya kifahari ambapo nchi hizi mbili zilianza mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja tangu mapambano ya kwenye mpaka yalipoanza na kuashiria kuingia kwenye vita kamili wiki saba zilizopita. Wizara za ulinzi na mambo ya ndani kutoka nchi hizo mbili zilikuwepo kwenye mazungumzo ambayo yalilenga juu ya masuala muhimu ya usalama.

Mazungumzo yanafanyika huku kukiwa na vitisho vya vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wanadiplomasia, waangalizi na wapatanishi walisema hali tulivu haikuwepo ikilinganishwa na raundi ya mazungumzo ya awali ambayo yalikwama mwezi April.

Wakati mkutano ukianza mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini Pagan Amum aliishutumu Khartoum kwa kudanganya kuhusu kuyaondoa majeshi yake yote kama ilivyopendekezwa na Umoja wa Mataifa kutoka kwenye mkoa wenye mzozo wa Abyei. Amum alisema Sudan bado ina makombora mawili ya nguvu huko Abyei.

Amum alisema Sudan Kusini ina nia ya dhati ya kuendelea na mazungumzo na kutekeleza matakwa ya jumuiya ya kimataifa. Lakini alisema anaona nafasi ndogo ya mafanikio katika mazungira ya sasa.

Wapatanishi wa Khartoum walikataa ombi la kufanyiwa mahojiano lakini msemaji Omer Dahab aliwaambia waandishi wa habari kuwa Sudan inashirikiana na wote Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika kufuata agizo la kuyaondoa majeshi yake.

Alipoulizwa kama anaweza kusema Sudan imeondoa majeshi yake yote na wanajeshi wengine nje ya Abyei, Dahab alijibu,“ndio ninaweza kusema hivyo”.

Haikuweza kufahamika mara moja kama kuwepo kwa “polisi katika eneo la mafuta” kutaangaliwa kama ukiukaji wa matakwa ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa kutaka kuondoa majeshi yote kutoka Abyei.

Mpatanishi wa jopo la Umoja wa Afrika linaloongozwa na Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki alithibitisha kwamba kamati ya uangalizi inatarajiwa kukutana Alhamisi.

XS
SM
MD
LG