Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:56

Kevin Spacey akutwa hana hatia katika kesi ya unyanyasaji wa kingono

Mwigizaji wa Marekani, Kevin Spacey, katikati, akiondoka Mahakamani siku ya Alhamisi, Oktoba 20, 2022, mjini New York.

Baraza la majaji hapa Marekani, jana lilikubaliana na Mcheza sinema Kevin Spacey, na kufikia uamuzi kuwa hakumnyanyasa kingono mwigizaji mwenzake Anthony Rapp katika miaka ya 1980. Wakati huo Rapp akiwa na umri wa miaka 14.

Hii inaleta hitimisho la jaribio ambalo lilitokana na vuguvugu la MeToo. Madai ya Rapp na wengine yalipelekea kusitishwa ghafla kwa taaluma ya mshindi huyo wa Tuzo za filam mara mbili Spacey.

Uamuzi huo Alhamisi ulikuja baada ya majaji kujadili kwa zaidi ya saa moja. Rapp alidai kuwa aliumizwa kisaikolojia baada ya Spacey kutaka kufanya mapenzi mwaka 1986. Spacey alishuhudia kwamba tukio hilo halikuwahi kutokea na alisema alikuwa na uhakika na hilo.

Uamuzi wa kesi hiyo ya madai ulikuja kwa kasi ya umeme. Majaji katika mahakama ya serikalu kuu huko New York walijadili kwa zaidi ya saa moja kabla ya kuamua kuwa Rapp hakuwa amethibitisha madai yake.

Rapp, ambaye sasa ana miaka 50, na Spacey, 63, kila mmoja alitoa ushahidi wake kwa siku kadhaa katika kesi hiyo ya wiki tatu.

XS
SM
MD
LG