Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 02:46

Kesi za ugonjwa usiofahamika kwa watoto imeongezeka:CDC inaripoti


Kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani-CDC
Kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani-CDC

Kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani-CDC kilisema idadi ya kesi za ugonjwa usiofahamika unadhoofisha viungo vya mwili kwa watoto umefikia rekodi ya juu mwaka huu

Kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani-CDC kilisema kwamba idadi ya kesi za ugonjwa usiofahamika ambao unadhoofisha viungo vya mwili kwa watoto umefikia rekodi ya juu mwaka huu.

CDC ilithibitisha Jumatatu kesi 24 zaidi za ugonjwa unaoathiri uti wa mgongo pamoja na sehemu za mishipa inayobeba ujumbe kupeleka na kurudisha kwenye ubongo kitaalamu AFM unaofanana na polio na kufikia idadi ya kesi 158 katika majimbo 36 mwaka 2018.

Maafisa wa afya Marekani bado hawafahamu nini kinachosababisha watoto kupoteza uwezo wa kutabasamu kwenye nyuso zao, kugeuza shingo zao au kugeuka nyuma, kutembeza mikono au miguu. Dalili hizo hujitokeza kiasi cha wiki moja baada ya mtoto kupata homa kali na tatizo la kupumua.

Hali hiyo inafananishwa na polio lakini maafisa wa afya wanasema hawajapata ushahidi AFM inauhusiano na polio ugonjwa ambao ulitokomezwa Marekani baada ya chanjo kupatikana katika miaka ya 1950. Kinachowapa wasi wasi maafisa ni kwamba watoto wengi wanaishia kupooza na baadhi yao huishia kulazwa hospitali katika vitengo vya huduma mahututi na kuwekewa mashine za kuwasaidia kupumua.

kulingana na idara ya afya Marekani ni kwamba CDC imekuwa ikifuatilia kesi za AFM tangu Agosti 2014. Tangu wakati huo kumekuwepo na kesi za AFM 484 zilizothibitishwa.

Wiki iliyopita CDC ilisema idadi ya kesi za ugonjwa huo mwaka huu inaonekana kuongezeka kama ilivyooneshwa na kupungua idadi ya wagonjwa ambao wamefanyiwa uchunguzi na uwezekano wa kuwa na AFM.

XS
SM
MD
LG