Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:39

Kesi za Covid 19 zaongezeka Uganda


Mchuuzi katika soko la Nakasero mjini Kampala Uganda akiwa amevaa barakoa na kushika mwamvuli.(Photo by SUMY SADURNI / AFP)
Mchuuzi katika soko la Nakasero mjini Kampala Uganda akiwa amevaa barakoa na kushika mwamvuli.(Photo by SUMY SADURNI / AFP)

Uganda inaona ongezeko kubwa la visa vya COVID-19, na kulazimisha maafisa wake wa afya kuchukua hatua kali za dharura. Kutoka kesi 200 kwa siku mwezi Aprili, nchi hiyo sasa inarekodi zaidi ya kesi 1,000 kwa siku wakati kuna uhaba wa chanjo unaokuja.

Katika Wizara ya Afya, mamia ya watu wamejipanga wakiwa wamesimama, wengine wameketi, wakati mstari unaelekea hema ya chanjo.

Kesi za COVID-19 nchini Uganda zimefikia 44,594, na vifo 361. Daktari Yonas Tegegn Wolde-mariam, mwakilishi wa nchi katika Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO anaelezea kiwango ambacho virusi vya corona vinaenea nchini Uganda.

Katika juma linaloanzia Aprili 25, Uganda iliripoti kesi 256. Wiki inayoanza Mei mbili, idadi hiyo iliongezeka hadi 411. Wiki ya Mei 9, idadi ilikwenda hadi 475. Na wiki ya Mei 16, idadi hiyo tayari imefikia 1,060.

Kampala ni kati ya wilaya 10 ambazo zimerekodi idadi kubwa ya visa.

Odoi Paul, mwenye umri wa miaka 39, ni miongoni mwa watu wengi waliofurika kwenye Wizara ya Afya Alhamisi kupata chanjo yao ya kwanza.

Odoi anasema “Ili kuhakikisha kuwa niko huru kutokana na COVID-19. Kama ilivyo India, watu wanakufa, na huko Marekani. Ndiyo sababu nasema, wacha mimi pia niende kuokoa maisha yangu kabla ya jambo kama hilo kutokea katika nchi yetu.

Daktari Henry Mwebesa, mkurugenzi wa huduma za afya, anabainisha kuwa imeichukua nchi chini ya siku 10 kufikia katika janga kamili.

Kundi lililoathiriwa zaidi ni watu wenye umri kati ya miaka 20 na 39, na idadi ya wagonjwa mahututi wa COVID-19 ni kubwa kuliko ilivyokuwa katika wimbi la kwanza.

Dakta Mwebesa anasema maafisa wanafanya maamuzi magumu kuhakikisha kuwa watu katika maeneo yenye watu wengi kama vile Kampala wanapata chanjo.

“Pia kutambua kwa wasiwasi kiasi kwamba wilaya nyingine, haswa katika mikoa ya Mashariki na Kaskazini, hazijafanya vyema pia. Kwa hivyo, kikao cha kamati ya mikakati katika Wizara ya Afya kiliamua kwamba chanjo ziondolewe kutoka wilaya ambazo hazifanyi vizuri, na kwamba zoezi hilo linapaswa kuanza tarehe 27 Mei, ambayo ni leo ”aliongeza Dokta Mwebesa.

Mwezi Machi, Uganda ilipokea dozi 964,000 za chanjo ya COVID-19 kutoka kwa kituo cha COVAX, na dozi 100,000 kutoka India. Tangu Machi 10, karibu watu 550,000 wamepewa chanjo ya AstraZeneca.

Sehemu ya pili ya chanjo ilitarajiwa kuanza mwezi huu. Lakini Dk Wolde-mariam anasema hiyo haina uhakika.

Kuonyesha kiwango kamili cha wimbi la pili, usiku wa alhamisi vituo vitatu vikubwa vya Televisheni nchini Uganda vilifanya matanagazo ya pamoja ya habari chini ya kauli mbiu, Chukua hatua au Uangamie.

/

XS
SM
MD
LG