Kesi ya Wakenya wanne mashuhuri itaanza kusikilizwa Aprili mwaka ujao kwa mashitaka kwamba walipanga ghasia zilizosababisha maafa makubwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ilisema jana kwamba kesi ya waziri wa zamani William Rutto na mkuu wa radio Joshua Arap Sang itaanza kusikilizwa Aprili 10. Kesi ya naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na mkuu wa zamani wa wafanyakazi wa serikali Francis Muthaura itaanza Aprili 11.
Watu hao wanne wanashitakiwa kwa kusaidia kupanga ghasia zilizozuka kote Kenya baada ya uchaguzi wa rais wa 2007.
Watu wapatao 1,300 waliuwawa na zaidi ya laki 3 kupoteza makazi yao katika mapigano na ghasia za kikabila.