Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 07:04

Kesi ya Mtanzania yaahirishwa NY


Picha ya zamani ya Ahmed Khalfan Ghailani, Mtanzania anayekabiliwa na kesi mjini New York.
Picha ya zamani ya Ahmed Khalfan Ghailani, Mtanzania anayekabiliwa na kesi mjini New York.

Kesi ya ugaidi ya Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani iliyokuwa ianze New York leo imeahirishwa.

Kesi ya Mtanzania Ahmed Khalfani Ghailani ambayo ni ya kwanza kusikilizwa katika mahakama ya kiraia kwa wafungwa waliokuwa Guantanamo Bay, Cuba, imeahirishwa mjini New York baada ya jaji wa mahakama moja ya serikali kuu kusema serikali haiwezi kumwita shahidi mmoja muhimu.

Jaji Lewis Kaplan alitangaza Jumatano kwamba shahidi anayeitwa Hussein Abebe hatoruhusiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya New York, katika kesi dhidi ya Ghailani. Kwa hiyo ameiahirisha kesi ili kutoa muda kwa upande wa mashtaka kukata rufaa. Maafisa wanasema Abebe alimuuzia milipuko Ghailani, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ulipuaji wa mabomu ya mwaka 1998, katika balozi mbili za Marekani, mjini Dar es Salaam na Nairobi.

Ghailani anashtakiwa kwa njama za mashambulizi ya mabomu huko yaliyotumika Kenya na Tanzania ambapo watu 224 waliuawa wakiwemo wamarekani 12. Kama akipatikana na hatia huenda akahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Marekani inasema Ghailani alikuwa akishikiliwa na kuhojiwa na maafisa wa shirika la ujasusi la marekani -CIA- kwa miaka miwili baada ya kukamatwa nchini Pakistan mwaka 2004. Baada ya kuwa chini ya ulinzi wa CIA, alihamishiwa na kupelekwa huko Guantanamo bay cuba.

Mawakili wa Ghailani wanadai kuwa kipindi kirefu cha kuwekwa kizuizini kimekiuka haki zake za msingi, lakini jaji alitupilia mbali madai hayo mwezi July, akisema Ghailani alikuwa akishikiliwa kwa ajili ya maslahi ya usalama wa taifa wa marekani.

XS
SM
MD
LG