Pakistan imegundua kesi yake ya kwanza ya Omicron aina mpya ya kirusi cha corona. Maafisa wa afya walisema leo Alhamis kwamba maambukizi hayo yalipatikana kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 57 ambaye hajachanjwa huko Karachi, jiji kubwa la nchi na mji mkuu wa mkoa wa kusini wa Sindh.
Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa mgonjwa huyo ambaye alikuwa amejitenga nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hakuwa na historia ya kusafiri na utaftaji wa mawasiliano na watu aliokutana nao ulikuwa unaendelea. Bado hatujahitimisha uchunguzi wa kina wa sampuli ya mgonjwa, lakini jinsi virusi vinavyofanya inaonekana kama ni Omicron alisema waziri wa afya katika mkoa huo Azra Fazal Pechuno kwenye taarifa ya video.
Pechuno alisema watu hawahitaji kuogopa na pia aliwasihi watu kupata chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona.